Mabao mawili ya Mbappé yaipandisha Real kileleni mwa msimamo wa ligi
Mabao mawili ya Kylian Mbappé yameipa Real Madrid ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Villarreal.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alianza kufunga mara baada ya kipindi cha pili kuanza, kisha akahakikisha ushindi wa pointi zote tatu kwa kufunga penalti ya dakika ya 92.
Ushindi huo umeifanya Los Blancos kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga) kwa tofauti ya pointi mbili, ingawa Barcelona inaweza kurejea kileleni endapo itashinda dhidi ya Real Oviedo siku ya Jumapili.