Msanii nguli wa Bongo Fleva na kiongozi wa Konde Gang, Harmonize, ametangaza kuachia wimbo wake mpya Ijumaa hii. Huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kazi hiyo mpya, Harmonize amehakikisha kuweka wazi kuwa wimbo huo hauna uhusiano wowote na mpenzi wake wa zamani.
Kupitia Insta Story yake, Harmonize alitoa ufafanuzi mzito, akisema:
“HAIHUSIANI NA X WANGU YEYOTE!!!
NINA HESHIMA KUBWA SANA KWAO WOTE.
KAMA NIKIMUIMBAJI X WANGU YEYOTE HAITOKUWA KAZI KUBWA KAMA MNAVYO DHANI! ILA NDO SIWEZI UPENDO WANGU UNAUPITILIZA NA KUWA KAMA KAKA MDOGO KWENYE FAMILIA.
SO HATA TIKTOKA TUMESHINDWA HESHIMA NA ADABU YANGU KWENYE FAMILIA INABAKI PALE PALE, SO HATA AKINIUNIKA TUNAKUTANA KWENYE VIKAO VYA FAMILIA 😂.
HIZI GOMA NI KWA NIABA YA XXX WOTE DUNIANI, MSINIPENDE KUAONA MNAYAWATA WAKWENU TUU KISA NIMEMBA MTE 😂 SEE YOU ON FRIDAY KUMEKUCHA!!!”
Harmonize Atoa Majibu kwa Wanaodhani Wimbo Unahusu Maisha Yake
Kwa kauli hiyo, Harmonize ameeleza kuwa hata kama angeamua kuimba kuhusu mmoja wa wapenzi wake wa zamani, hilo halingekuwa jambo gumu. Hata hivyo, anasisitiza kuwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu heshima na upendo wake kwao umebadilika na kuwa wa kifamilia.
Related: Harmonize – Mama ni Mama
Pia, ameweka wazi kuwa wimbo huu hauzungumzii mahusiano yake binafsi bali unawakilisha watu wote walioachana na wapenzi wao. Kwa maneno mengine, wimbo huu ni kwa niaba ya wale wote waliohisi maumivu ya mapenzi au waliowahi kupitia kipindi kigumu cha mahusiano.
Mashabiki Wasubiri Kwa Hamu
Wimbo huu unatarajiwa kuachiwa rasmi Ijumaa hii, na mashabiki wa Konde Gang wanatarajia kuona ujumbe uliobebwa na kazi hiyo mpya. Je, Harmonize anatoa jibu la kutosha kwa wale wanaodhani kwamba nyimbo zake zimebeba simulizi za maisha yake binafsi?
Tupe maoni yako na kaa tayari kwa wimbo mpya kutoka kwa Harmonize!